Saturday, October 28, 2017

MWIKALO CUP

Mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la 'MWIKALO CUP', yanatarajiwa kuanza mwezi wa 12 kwa mfumo wa ligi ambayo yatafanyika wilayani Handeni katika uwanja wa Azimio uliopomjini hapo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanzilishi wa ligi hiyo Haji Sedenga Mwikalo, amesema kwa sasa yeye na chama cha mpira wa miguu wilayani hapo HDFA, wanaendelea na mazungumzo ya pamoja kuangalia jinsi gani ligi iyo itakavyo endeshwa wilayani hapo, Mwikalo alikuwa akisema kuwa, anafikiria kuiendesha ki- kalenda akiwa na maana kuwa kila ifikapo mwezi wa disemba ya kila mwaka itakuwa fursa ya vijana wilayani hapo kuweza kushiriki ligi hiyo kwa kutumia mfumo wa vilabu vya mpira au, vilabu vya mpira kutoka kila kata za wilaya nzima ya Handeni, hayo wanazungumza na chama cha mpira wilayani hapo ikiwa imesalia takribani mwezi mmoja ligi hiyo kuanza.

Aliendelea akisema kuwa anafikiria kuitengeneza ligi hiyo kuwa ya aina yake katika wilaya hiyo kwa sababu zifuatazo, hali ya michezo wilayani hapo imekuwa duni na vijana sasa hawana fursa ya kuonyesha vipaji vya michezo huku akijua kuwa anaamini vipaji vipo na ni lazima vitafutiwe sehemu ya kuvionyesha hasa pale scouts wa kutafuta wachezaji watakapo fika kuangalia wachezaji wanaowahitaji kuwasajili katika timu kubwa ili kuendeleza vipaji vyao na kuchukulia mpira kama ajira rasmi.

Ndugu Mwikalo amewasihi timu mbali mbali wilayani hapo kuchukua fursa hii ya ligi ya mwikalo kama sehemu muhimu kwao ya kuonyesha vipaji vyao kwani hawajui nani atakuwepo na ni mchezaji gani atapata fursa rasmi ya kuendelea mbele katika timu kubwa na pengine kufungua mlango sasa kwa handeni kupata wachezaji wazuri nje ya mipaka yetu ya nchi. Pia ligi hiyo inatizamiwa hapo baadae kualika timu nyingine nje ya mipaka ya wilaya hiyo kama vile timu kutoka wilaya ya Korogwe na Kilindi kama chachu ya kuanza kukuza michezo rasmi wilayani hapo. Kwa kila mwaka tutajaribu kuikuza na kuleta aidia na mipango mipya ya kubolesha ligi yetu, tusingependa iishie michezoni tu, pia itakuwa taasisi ya kusaidia jamii kwa njia moja au nyingine kiuwezeshaji na kiusafi wa mazingira yetu, lazima tuwe na mifumo mipya mizuri ya kuigwa ili vijana wapate ajira na waeke mazingira salama ili tuweze kuishi kisasa zaidi kwa kwa ukaribu zaidi ili tusaidiane.

Habari kamili za ratiba ya ligi ya MWIKALO CUP, itatolewa hapo baadae kupitia blog ya mwikalo.blogspot.com na katika magazeti ambayo yatatajwa hapo baadae.





0 comments:

Post a Comment