Tuesday, October 10, 2017

MOHAMED SALAH

EGYPT- MISRI.

Mchezaji wa timu ya taifa Mohamed Salah ameiwezesha timu yake ya taifa Misri kuibuka na ushindi katika mchezo wa kombe la dunia mwaka 2018. Salah ambaye pia ni mchezaji wa club ya Liverpool na inchini Uingereza alifunga magoli mawili hiku moja likiwa la mkwaju wa penati.

Mchezo huo ulioluwa na ushindani wa kila timu kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia mwakani, Misri iliwaarika timu ya taifa ya Congo mpaka dakika 90 za mchezo huo Misri 2-1 Congo.

Misri itaungana na timu zingine balani Ulaya katika kushiriki katika mashindano hayo makubwa ulimwenguni. Hii imekuwa jambo lililotarajiwa sana na wapenzi wa mpira na raia wote kwa ujumla nchini Misri kuingia katika mashindano ya kombe la dunia.

 Wachezaji walionesha nia ya kusaka ushindi kwa kila mechi waliocheza na mwisho wa yote timu hiyo imeweza kuingia katika mashindano ya kombe la dunia ambayo yanatarajiwa kuchezwa mwakani mwaka 2018 inchini Urusi.


0 comments:

Post a Comment