Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Paul Pogba atakuwa nje ya uwanja kwa mda mrefu kidogo kutokana na majeraha aliyoyapata mwezi uliopita katika mchezo dhidi ya Basel. Pogba ni mchezaji ambaye ameisaidia Man United kupata ushindi katika mechi kadhaa katika ligi kuu ya England na Mashindano ya Uefa Champion League.
Mchango wake unaonekana hasa pale kwenye nafasi ya kiungo alipokuwa akicheza kwa kujiamini na kufanya juhudi binafsi ili timu yake iweze kuibuka na ushindi, kukosekana kwa Paul Pogba katika kikosi cha Man U hakuna athari yoyote iliyotokea kufuatia kutokuwepo kwake katika kikosi hicho.
Man United wameshinda mechi tano mfululizo bila ya kuwa na Pogba hii inaonyesha kuwa Man United bado wako zivuri katika safu ya kiungo. Kuna wachezaji wazuri wanaoweza kucheza nafasi ya Pogba kama vile Matic, Felaini na wengine.
0 comments:
Post a Comment