Tuesday, October 31, 2017

HDFA HANDENI

HDFA HANDENI

MAOMBI.


CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA HANDENI HDFA.
P. O BOX 350
HANDENI. TANGA.
YAH: OMBI LA MAANDALIZI YA LIGI YA MWIKALO CUP.
Kwa Mwenyekiti na Katibu wa chama chetu cha mpira wa miguu wilaya ya Handeni, husika na somo hapo juu la maandalizi ya kiwanja cha michezo na mwaliko wa vilabu vya mchezo wa mpira wa miguu wilayani Handeni na wilaya za jirani.
Mwangalizi wa kampuni ya Biashara ya Mwikalo enterprise, Ndugu Haji Sedenga Mwikalo, amewaomba chama hicho cha HDFA kuandaa ligi hiyo ambayo inatazamiwa kuanza mwezi wa 12 mwaka 2017 wilayani hapo kwa mujibu wa mipango ya HDFA watakavyoipanga kulingana na taratibu zao za kiutendaji wa kimichezo wilayani hapo.
Sisi Mwikalo tupo tayari kimaandalizi na sasa tunasubiri maelekezo ya chama chetu cha HDFA kutupatia maelekezo ya kiwanja, timu zitakazo shiriki na mfumo wa ligi hiyo itakavyoandaliwa kimazingira ya kimichezo wilayani hapo…tutashukuru kwa msaada wenu.
Mwikalo cup, inatazamia kusimamia vifaa vya maandalizi… kama vile barua za mwaliko wa vilabu, barua za maombi ya viwanja au kiwanja, barua za mialiko ya viongozi ikibidi, barua za mawakala wa kuja kuangalia vipaji wilayani hapo na mengineyo.
ZAWADI.
Mpaka sasa, Mwikalo haijaweka wazi zawadi zitakazoandaliwa, lakini moja ya zawadi kubwa inayotarajiwa kwa timu zote ni kuja kwa mawakala wa michezo kuangalia wachezaji wa kusajiri katika vilabu vya ngazi za juu. Pia uhakika wa jezi za Mwikalo cup, pea moja itakabidhiwa kwa mshindi siku ya fainali, na bado tunatafakali mambo mengine yatakayotoa faraja kwa timu zetu.
Tunatanguliza shukurani zetu za dhati mapema kwa kutuongoza katika maandalizi haya ya mapema. Mwikalo ipo tayari kwa ushauri zaidi katika kuleta mafanikiyo haya ya kuendeleza michezo wilayani kwetu. Shukrani.
Mkurugenzi: Haji Sedenga Mwikalo.
FLAT - HANDENI

FLAT - HANDENI



CHAMA CHA WAAMUZI WA MPIRA WA MIGUU FRAT-HANDENI.
YAH: MWALIKO NA UTAMBULISHO WA KOMBE LA MWIKALO.
Kampuni ya Mwikalo, inajitambulisha rasmi kwenu kwa kuanzisha ligi ya Mwikalo ambaya inategemea kufanyika kila mwaka ifikapo disemba. Dhumuni la ligi hiyo au kombe hilo ni kutoa hamasa kwa mchezo wa mpira wa miguu wilayani hapo, kutafuta njia mbadala ya kukuza vipaji na kuwatafutia timu kubwa kama ajira za michezo kwa kutumia mawakala ambao tunatizamia kuwapata mara kwa mara katika ligi yetu na ligi nyingine ambazo tutafahamishwa ili kukuza michezo wilayani kwetu.
Dhumuni kubwa kwa barua hii, ni kuomba msaada wa ushirikiano kwenu nyie waamuzi wetu, kwani tuna fahamu bila msaada wenu itatuwia vigumu kwetu.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwenu, pia tunaomba msaada wa mawazo yenu kwetu, sisi Mwikalo tunaamini ushirikiano wa pamoja ndio njia ya mafanikio ya kila Nyanja katika kila jambo lolote lile hapa duniani, hivyo hatutawaacha nyuma ndugu zetu waamuzi.
Tutashukuru sana kwa Msaada wa Mawazo yenu,
ASANTENI.
Haji S Mwikalo.

Saturday, October 28, 2017

MWIKALO CUP

Mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la 'MWIKALO CUP', yanatarajiwa kuanza mwezi wa 12 kwa mfumo wa ligi ambayo yatafanyika wilayani Handeni katika uwanja wa Azimio uliopomjini hapo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanzilishi wa ligi hiyo Haji Sedenga Mwikalo, amesema kwa sasa yeye na chama cha mpira wa miguu wilayani hapo HDFA, wanaendelea na mazungumzo ya pamoja kuangalia jinsi gani ligi iyo itakavyo endeshwa wilayani hapo, Mwikalo alikuwa akisema kuwa, anafikiria kuiendesha ki- kalenda akiwa na maana kuwa kila ifikapo mwezi wa disemba ya kila mwaka itakuwa fursa ya vijana wilayani hapo kuweza kushiriki ligi hiyo kwa kutumia mfumo wa vilabu vya mpira au, vilabu vya mpira kutoka kila kata za wilaya nzima ya Handeni, hayo wanazungumza na chama cha mpira wilayani hapo ikiwa imesalia takribani mwezi mmoja ligi hiyo kuanza.

Aliendelea akisema kuwa anafikiria kuitengeneza ligi hiyo kuwa ya aina yake katika wilaya hiyo kwa sababu zifuatazo, hali ya michezo wilayani hapo imekuwa duni na vijana sasa hawana fursa ya kuonyesha vipaji vya michezo huku akijua kuwa anaamini vipaji vipo na ni lazima vitafutiwe sehemu ya kuvionyesha hasa pale scouts wa kutafuta wachezaji watakapo fika kuangalia wachezaji wanaowahitaji kuwasajili katika timu kubwa ili kuendeleza vipaji vyao na kuchukulia mpira kama ajira rasmi.

Ndugu Mwikalo amewasihi timu mbali mbali wilayani hapo kuchukua fursa hii ya ligi ya mwikalo kama sehemu muhimu kwao ya kuonyesha vipaji vyao kwani hawajui nani atakuwepo na ni mchezaji gani atapata fursa rasmi ya kuendelea mbele katika timu kubwa na pengine kufungua mlango sasa kwa handeni kupata wachezaji wazuri nje ya mipaka yetu ya nchi. Pia ligi hiyo inatizamiwa hapo baadae kualika timu nyingine nje ya mipaka ya wilaya hiyo kama vile timu kutoka wilaya ya Korogwe na Kilindi kama chachu ya kuanza kukuza michezo rasmi wilayani hapo. Kwa kila mwaka tutajaribu kuikuza na kuleta aidia na mipango mipya ya kubolesha ligi yetu, tusingependa iishie michezoni tu, pia itakuwa taasisi ya kusaidia jamii kwa njia moja au nyingine kiuwezeshaji na kiusafi wa mazingira yetu, lazima tuwe na mifumo mipya mizuri ya kuigwa ili vijana wapate ajira na waeke mazingira salama ili tuweze kuishi kisasa zaidi kwa kwa ukaribu zaidi ili tusaidiane.

Habari kamili za ratiba ya ligi ya MWIKALO CUP, itatolewa hapo baadae kupitia blog ya mwikalo.blogspot.com na katika magazeti ambayo yatatajwa hapo baadae.





Tuesday, October 10, 2017

LIONEL MESSI ( FIFA WORLD CUP RUSSIAN 2018)

ARGENTINA.

Timu ya taifa ya Argentina imefuzu kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia mwakani huko Urusi. Argentina ailikuwa inatafuta  nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo ikicheza mchezo wao wa mwisho wa kutafuta nafasi ya kuendelea na mashindano ya kombe la dunia 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Ecuador.

Mchezo huo ambao ulikuwa unaamua ni timu gani iendelee na mashindano hayo na timu gani ibaki, mpaka mwisho wa mchezo huo ilikuwa ni timu ya Argentina ikipata ushindi wa magoli 3 na timu ya Ecoudor wakipata goli 1.





Mchezaji wa timu ya Barcelona na timu taifa ya Argentina Lionel Messi aliibuka kuwa shujaa juu ya timu yake hii ni baada ya kuifungia magoli matatu muhimu katika mchezo huo.

Ecoudor ilikuwa nyumbani kuikaribisha timu ya Argentina. Argentina itaungana na timu zingine za taifa kama vile:-
  •  Misri.
  •  England.
  •  Brazil.
  •  Ureno.
  •  France 
Hizo ni baadhi ya timu zilizofuzu kushiriki kucheza kombe la dunia ( FIFA WORLD CUP RUSSIAN 2018)