Thursday, September 7, 2017

WILAYA YA HANDENI

Wilaya ya Handeni ni moja kati ya wilaya nane zilizopo katika mkoa wa Tanga. Wilaya Handeni ni moja ya wilaya nyingi Tanzania ambazo zinachangia Taifa kwa kilimo kikubwa cha mahindi na mazao mengine ya chakula na biashara, kama Maharage, Choroko, Kunde, Mbaazi, Mihogo, Viazi vitamu na Viazi mviringo pamoja na matanda. Pia wilaya hii inajishughulisha na mifugo kwa kiasi kikubwa, ina wafugaji wa kuku wa kienyeji, na wale wa kisasa. Pia ufugaji wa ng'ombe mbuzi na kondoo upo kwa kiasi kikubwa na kufanya kuwapo na soko la minada ya kununua mifugo vile vile kuchoma nyama katika siku za minada. Kimtazamo, Handeni kwa ujumla imetazamiwa kuwa na idadi ya watu wapatao 300,000 mpaka 400,000 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2017, na hii inajumuisha majimbo yote mawili katika wilaya.

 Handeni ina majimbo mawili na kufanya idadi ya kata kugawanywa kutokana na ukubwa wa wilaya yenyewe. Majimbo hayo ni Handeni Mji, ambayo ina kata 12, halkadhalika na Handeni Vijijini ambayo ina kata 21. Tokea Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 wilaya ya Handeni kwa ujumla imepata kuongozwa na wabunge 5 hadi kufikia mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment