Saturday, September 23, 2017

Neymar vs Cavani

Kutoka Ufaransa.

Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa PSG imecheza mchezo wao dhidi ya Lyon. Katika mchezo huo umetokea mtafaruku kati ya wachezaji wao wawili Neymar na Cavani. Pulukushani hizo zimetokea baada ya kila mmoja akitaka kupiga mipira ya adhabu na penati. Hii imaonyesha kuwa wachezaji hao hawakuwa na mawasiliano mazuri katika mchezo huo dhidi ya Lyon.

Baada ya PSG kupata penati alionekana Neymar alitaka kupiga penati ile lakin Cavani tayari alikuwa ameushika mpira akimaanisha kuwa nae anahitaji kupiga penati. Neymar alionekana kutoridhia maamuzi yale ya Cavani licha ya Cavani kukosa penati hiyo.

Angalia video hii fupi ikionesha pulukushani hiyo kati ya Neymar na Cavani.








0 comments:

Post a Comment